Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 101.8
Bible en Swahili de l’est


1 Rehema na hukumu nitaziimba, Ee Bwana, nitakuimbia zaburi.Psaumes 89.1 Psaumes 71.22-71.23 Apocalypse 19.1-19.3 Psaumes 51.14 Psaumes 97.8
2 Nitaiangalia njia ya unyofu; Utakuja kwangu lini? Nitakwenda kwa unyofu wa moyo Ndani ya nyumba yangu.1 Rois 9.4 Psaumes 119.106 Psaumes 119.115 Psaumes 40.17 Psaumes 101.6
3 Sitaweka mbele ya macho yangu Neno la uovu. Kazi yao waliopotoka naichukia, Haitaambatana nami.Job 31.1 Proverbes 6.25 Psaumes 119.37 2 Samuel 11.2-11.3 Matthieu 5.28
4 Moyo wa ukaidi utaondoka kwangu, Lililo ovu sitalijua.Proverbes 11.20 Proverbes 3.32 Matthieu 7.23 2 Corinthiens 6.14-6.16 2 Timothée 2.19
5 Amsingiziaye jirani yake kwa siri, Huyo nitamharibu. Mwenye macho ya kiburi na moyo wa majivuno, Huyo sitavumilia naye.Psaumes 18.27 Psaumes 50.20 Proverbes 30.13 Psaumes 15.3 Psaumes 10.2-10.4
6 Macho yangu yatawaelekea waaminifu katika nchi, Hao wakae nami. Yeye aendaye katika njia kamilifu, Ndiye atakayenitumikia.Apocalypse 21.3 Luc 12.43-12.44 Romains 13.1-13.4 Philippiens 3.12-3.15 Psaumes 34.15
7 Hatakaa ndani ya nyumba yangu Mtu atendaye hila. Asemaye uongo hatathibitika Mbele ya macho yangu.Actes 1.25 Proverbes 29.12 Psaumes 52.2 Actes 1.16-1.20 2 Samuel 4.10-4.12
8 Asubuhi hata asubuhi nitawaharibu Wabaya wote wa nchi. Niwatenge wote watendao uovu Na mji wa Bwana.Psaumes 75.10 Jérémie 21.12 Psaumes 48.8 Psaumes 48.2 Osée 9.3

Cette Bible est dans le domaine public.