Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 101.2
Bible en Swahili de l’est


1 Rehema na hukumu nitaziimba, Ee Bwana, nitakuimbia zaburi.Psaumes 89.1 Psaumes 71.22-71.23 Apocalypse 19.1-19.3 Psaumes 145.7 Psaumes 103.6-103.8
2 Nitaiangalia njia ya unyofu; Utakuja kwangu lini? Nitakwenda kwa unyofu wa moyo Ndani ya nyumba yangu.1 Rois 9.4 Psaumes 119.106 Psaumes 119.115 Psaumes 143.7-143.8 1 Samuel 18.14-18.15
3 Sitaweka mbele ya macho yangu Neno la uovu. Kazi yao waliopotoka naichukia, Haitaambatana nami.Job 31.1 2 Samuel 11.2-11.3 Proverbes 6.25 Psaumes 119.37 Matthieu 5.28
4 Moyo wa ukaidi utaondoka kwangu, Lililo ovu sitalijua.Proverbes 11.20 Proverbes 22.24 2 Corinthiens 11.33 Proverbes 2.12-2.15 Proverbes 3.32
5 Amsingiziaye jirani yake kwa siri, Huyo nitamharibu. Mwenye macho ya kiburi na moyo wa majivuno, Huyo sitavumilia naye.Psaumes 18.27 Psaumes 50.20 Proverbes 30.13 Psaumes 15.3 Proverbes 20.19
6 Macho yangu yatawaelekea waaminifu katika nchi, Hao wakae nami. Yeye aendaye katika njia kamilifu, Ndiye atakayenitumikia.Romains 13.1-13.4 Apocalypse 21.3 Luc 12.43-12.44 Proverbes 29.2 Philippiens 3.12-3.15
7 Hatakaa ndani ya nyumba yangu Mtu atendaye hila. Asemaye uongo hatathibitika Mbele ya macho yangu.Actes 1.25 Proverbes 29.12 Psaumes 52.2 Actes 1.16-1.20 2 Samuel 4.10-4.12
8 Asubuhi hata asubuhi nitawaharibu Wabaya wote wa nchi. Niwatenge wote watendao uovu Na mji wa Bwana.Psaumes 75.10 Psaumes 48.8 Jérémie 21.12 Psaumes 48.2 Apocalypse 22.14-22.15

Cette Bible est dans le domaine public.