Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

1 Chroniques 22.5
Bible en Swahili de l’est


1 Ndipo Daudi akasema, Hii ndiyo nyumba ya Bwana Mungu, na hii ndiyo madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa kwa Israeli.2 Chroniques 3.1 1 Chroniques 21.18-21.28 Genèse 28.17 2 Samuel 24.18 Psaumes 78.60
2 Basi Daudi akaamuru wakusanyike wageni waliokuwa katika nchi ya Israeli; akaweka waashi wachonge mawe ili kujenga nyumba ya Mungu.2 Chroniques 2.17 1 Rois 9.20-9.21 1 Rois 5.17-5.18 Ephésiens 2.12 1 Rois 7.9-7.12
3 Daudi akaweka akiba tele ya chuma kwa misumari ya tarabe za malango, na kwa mafungo; na ya shaba akiba tele isiyo na uzani;1 Chroniques 22.14 1 Chroniques 29.2 1 Rois 7.47 1 Chroniques 29.7 Jérémie 52.20
4 na mierezi isiyo na idadi; kwa kuwa Wasidoni na watu wa Tiro wakamletea Daudi mierezi tele.1 Rois 5.6-5.10 2 Chroniques 2.3 Esdras 3.7 2 Samuel 5.11
5 Daudi akasema, Sulemani mwanangu akali ni mchanga bado, na mwororo, nayo nyumba atakayojengewa Bwana haina budi kuwa nzuri mno, yenye sifa na yenye fahari katika nchi zote; kwa hiyo mimi nitaiwekea akiba. Basi Daudi akaweka akiba tele kabla hajafa.1 Rois 3.7 1 Chroniques 29.1 2 Pierre 1.13-1.15 2 Chroniques 7.21 Aggée 2.3
6 Ndipo akamwita Sulemani mwanawe, akamwagiza amjengee Bwana, Mungu wa Israeli, nyumba.Deutéronome 31.23 Actes 20.25-20.31 Deutéronome 31.14 1 Timothée 5.21 Matthieu 28.18-28.20
7 Daudi akamwambia Sulemani mwanawe, Kwangu mimi nia yangu ilikuwa kujenga nyumba kwa ajili ya jina la Bwana, Mungu wangu.Deutéronome 12.5 Deutéronome 12.11 Psaumes 132.5 2 Chroniques 2.4 Deutéronome 12.21
8 Lakini neno la Bwana likanijia, kusema, Wewe umemwaga damu nyingi, na vita vikubwa umevifanya; wewe hutajenga nyumba kwa ajili ya jina langu, kwa sababu umemwaga damu nyingi juu ya nchi machoni pangu;1 Chroniques 28.3 1 Rois 5.3 2 Samuel 7.5-7.11 Nombres 31.24 Nombres 31.20
9 tazama, utazaliwa mwana, atakayekuwa mtu wa kustarehe; nami nitamstarehesha mbele ya adui zake pande zote; kwani jina lake litakuwa Sulemani, nami nitawapa Israeli amani na utulivu siku zake ;1 Rois 4.25 1 Rois 5.4 1 Rois 4.20 2 Samuel 12.24-12.25 Esaïe 26.12
10 huyo ndiye atakayejenga nyumba kwa ajili ya jina langu; naye atakuwa mwanangu, nami nitakuwa babaye; nami nitakifanya imara milele kiti cha ufalme wake juu ya Israeli.2 Samuel 7.13-7.14 Hébreux 1.5 Esaïe 9.7 1 Rois 5.5 Psaumes 89.36-89.37
11 Sasa mwanangu, Bwana na awe pamoja nawe; ukafanikiwe, na kuijenga nyumba ya Bwana, Mungu wako, kama alivyonena kwa habari zako.1 Chroniques 22.16 Matthieu 1.23 Esaïe 26.12 Matthieu 28.20 1 Chroniques 28.20
12 Bwana na akupe busara na akili, akakuagizie juu ya Israeli; ili uishike torati ya Bwana, Mungu wako.2 Chroniques 1.10 1 Rois 3.9-3.12 Psaumes 72.1 Proverbes 2.6-2.7 1 Rois 11.1-11.10
13 Ndipo utakapofanikiwa, ukiangalia kuzitenda amri, na hukumu, Bwana alizomwagizia Musa juu ya Israeli; uwe hodari, na wa moyo mkuu; usiogope wala usifadhaike.1 Chroniques 28.20 1 Chroniques 28.7 Josué 1.6-1.9 1 Rois 2.3 Deutéronome 31.6-31.8
14 Basi sasa, tazama, katika shida yangu, nimeiwekea akiba nyumba ya Bwana, talanta elfu mia za dhahabu, na talanta elfu elfu za fedha; na shaba na chuma isiyo na uzani; kwa vile zilivyo tele; miti tena na mawe nimeweka akiba, nawe utaweza kuongeza.1 Chroniques 22.3 Jérémie 52.20 1 Chroniques 29.4-29.7 2 Corinthiens 8.2 1 Rois 10.14
15 Tena kwako kuna mafundi wengi, wenye kuchonga na kufanyiza kazi ya mawe na miti, na kila aliye mstadi kwa kazi yo yote;Exode 35.32 Exode 31.3-31.5 Exode 35.35 1 Rois 7.14 Exode 28.6
16 ya dhahabu, ya fedha, na ya shaba, na ya chuma, hapana hesabu; basi inuka ushike kazi, naye Bwana na awe pamoja nawe.1 Chroniques 22.11 1 Corinthiens 15.58 2 Chroniques 20.17 1 Samuel 17.37 1 Samuel 20.13
17 Tena Daudi akawaamuru wakuu wote wa Israeli, kwamba wamsaidie Sulemani mwanawe, akisema,1 Chroniques 28.1-28.6 1 Chroniques 29.6 Romains 16.2-16.3 Philippiens 4.3 3 Jean 1.8
18 Je! Si Bwana, Mungu wenu, aliye pamoja nanyi? Na kuwastarehesha pande zote? Kwa kuwa wenyeji wa nchi amewatia mkononi mwangu; nayo nchi imetiishwa mbele za Bwana, na mbele ya watu wake.1 Chroniques 23.25 1 Chroniques 22.9 2 Samuel 7.1 Josué 23.1 Deutéronome 12.10-12.11
19 Basi sasa jitieni moyo na nia kumtafuta Bwana, Mungu wenu; inukeni basi, mkamjengee Bwana Mungu mahali patakatifu, ili kulileta sanduku la agano la Bwana, na vyombo vitakatifu vya Mungu, ndani ya nyumba itakayojengwa kwa ajili ya jina la Bwana.1 Chroniques 28.9 1 Chroniques 22.7 2 Chroniques 5.7 Deutéronome 4.29 1 Rois 8.6

Cette Bible est dans le domaine public.