Préparatifs pour la construction du temple
 1  Ndipo Daudi akasema, Hii ndiyo nyumba ya Bwana Mungu, na hii ndiyo madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa kwa Israeli. 
2 Chroniques 3.1  1 Chroniques 21.18-21.28  Genèse 28.17  Jean 4.20-4.22  Psaumes 132.13-132.14  
 2  Basi Daudi akaamuru wakusanyike wageni waliokuwa katika nchi ya Israeli; akaweka waashi wachonge mawe ili kujenga nyumba ya Mungu. 
1 Rois 5.17-5.18  2 Chroniques 2.17  1 Rois 9.20-9.21  2 Rois 22.6  1 Chroniques 14.1  
 3  Daudi akaweka akiba tele ya chuma kwa misumari ya tarabe za malango, na kwa mafungo; na ya shaba akiba tele isiyo na uzani; 
1 Chroniques 22.14  1 Chroniques 29.2  1 Rois 7.47  1 Chroniques 29.7  Jérémie 52.20  
 4  na mierezi isiyo na idadi; kwa kuwa Wasidoni na watu wa Tiro wakamletea Daudi mierezi tele. 
1 Rois 5.6-5.10  2 Chroniques 2.3  Esdras 3.7  2 Samuel 5.11  
 5  Daudi akasema, Sulemani mwanangu akali ni mchanga bado, na mwororo, nayo nyumba atakayojengewa Bwana haina budi kuwa nzuri mno, yenye sifa na yenye fahari katika nchi zote; kwa hiyo mimi nitaiwekea akiba. Basi Daudi akaweka akiba tele kabla hajafa. 
1 Rois 3.7  1 Chroniques 29.1  1 Rois 9.8  Jean 4.37-4.38  Ecclésiaste 9.10  
 6  Ndipo akamwita Sulemani mwanawe, akamwagiza amjengee Bwana, Mungu wa Israeli, nyumba. 
1 Timothée 6.13-6.17  Nombres 27.18-27.19  Deutéronome 31.23  Actes 20.25-20.31  Deutéronome 31.14  
 7  Daudi akamwambia Sulemani mwanawe, Kwangu mimi nia yangu ilikuwa kujenga nyumba kwa ajili ya jina la Bwana, Mungu wangu. 
Psaumes 132.5  Deutéronome 12.5  Deutéronome 12.11  1 Rois 9.3  1 Rois 8.16-8.20  
 8  Lakini neno la Bwana likanijia, kusema, Wewe umemwaga damu nyingi, na vita vikubwa umevifanya; wewe hutajenga nyumba kwa ajili ya jina langu, kwa sababu umemwaga damu nyingi juu ya nchi machoni pangu; 
1 Chroniques 28.3  1 Rois 5.3  2 Samuel 7.5-7.11  Nombres 31.24  Nombres 31.20  
 9  tazama, utazaliwa mwana, atakayekuwa mtu wa kustarehe; nami nitamstarehesha mbele ya adui zake pande zote; kwani jina lake litakuwa Sulemani, nami nitawapa Israeli amani na utulivu siku zake ; 
1 Rois 4.25  1 Rois 5.4  1 Rois 4.20  2 Samuel 12.24-12.25  Aggée 2.9  
 10  huyo ndiye atakayejenga nyumba kwa ajili ya jina langu; naye atakuwa mwanangu, nami nitakuwa babaye; nami nitakifanya imara milele kiti cha ufalme wake juu ya Israeli. 
2 Samuel 7.13-7.14  Hébreux 1.5  Zacharie 6.12-6.13  1 Chroniques 17.12-17.14  Esaïe 9.7  
 11  Sasa mwanangu, Bwana na awe pamoja nawe; ukafanikiwe, na kuijenga nyumba ya Bwana, Mungu wako, kama alivyonena kwa habari zako. 
1 Chroniques 22.16  Matthieu 1.23  Esaïe 26.12  Matthieu 28.20  1 Chroniques 28.20  
 12  Bwana na akupe busara na akili, akakuagizie juu ya Israeli; ili uishike torati ya Bwana, Mungu wako. 
2 Chroniques 1.10  1 Rois 3.9-3.12  Psaumes 72.1  Deutéronome 4.6  Jacques 1.5  
 13  Ndipo utakapofanikiwa, ukiangalia kuzitenda amri, na hukumu, Bwana alizomwagizia Musa juu ya Israeli; uwe hodari, na wa moyo mkuu; usiogope wala usifadhaike. 
1 Chroniques 28.20  1 Chroniques 28.7  Josué 1.6-1.9  2 Timothée 2.1  Jérémie 22.3-22.4  
 14  Basi sasa, tazama, katika shida yangu, nimeiwekea akiba nyumba ya Bwana, talanta elfu mia za dhahabu, na talanta elfu elfu za fedha; na shaba na chuma isiyo na uzani; kwa vile zilivyo tele; miti tena na mawe nimeweka akiba, nawe utaweza kuongeza. 
1 Chroniques 22.3  Jérémie 52.20  1 Chroniques 29.4-29.7  2 Corinthiens 8.2  1 Rois 10.14  
 15  Tena kwako kuna mafundi wengi, wenye kuchonga na kufanyiza kazi ya mawe na miti, na kila aliye mstadi kwa kazi yo yote; 
Exode 35.32  Exode 31.3-31.5  Exode 35.35  1 Rois 7.14  Exode 28.6  
 16  ya dhahabu, ya fedha, na ya shaba, na ya chuma, hapana hesabu; basi inuka ushike kazi, naye Bwana na awe pamoja nawe. 
1 Chroniques 22.11  1 Chroniques 22.14  Josué 1.9  Juges 18.9-18.10  Juges 4.14  
 17  Tena Daudi akawaamuru wakuu wote wa Israeli, kwamba wamsaidie Sulemani mwanawe, akisema, 
1 Chroniques 28.1-28.6  1 Chroniques 29.6  Romains 16.2-16.3  Philippiens 4.3  3 Jean 1.8  
 18  Je! Si Bwana, Mungu wenu, aliye pamoja nanyi? Na kuwastarehesha pande zote? Kwa kuwa wenyeji wa nchi amewatia mkononi mwangu; nayo nchi imetiishwa mbele za Bwana, na mbele ya watu wake. 
1 Chroniques 23.25  1 Chroniques 22.9  2 Samuel 7.1  Josué 23.1  Josué 10.42  
 19  Basi sasa jitieni moyo na nia kumtafuta Bwana, Mungu wenu; inukeni basi, mkamjengee Bwana Mungu mahali patakatifu, ili kulileta sanduku la agano la Bwana, na vyombo vitakatifu vya Mungu, ndani ya nyumba itakayojengwa kwa ajili ya jina la Bwana. 
1 Chroniques 28.9  1 Rois 8.6  1 Chroniques 22.7  2 Chroniques 5.7  Deutéronome 4.29