Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 87.5
Bible en Swahili de l’est


1 Msingi wake upo Juu ya milima mitakatifu. 2 Bwana ayapenda malango ya Sayuni Kuliko maskani zote za Yakobo. 3 Umetajwa kwa mambo matukufu, Ee Mji wa Mungu. 4 Nitataja Rahabu na Babeli Miongoni mwao wanaonijua. Tazama Filisti, na Tiro, na Kushi; Huyu alizaliwa humo. 5 Naam, mintarafu Sayuni itasemwa, Huyu na huyu alizaliwa humo. Na Yeye Aliye juu Ataufanya imara. 6 Bwana atahesabu, awaandikapo mataifa, Huyu alizaliwa humo. 7 Waimbao na wachezao na waseme, Visima vyangu vyote vimo mwako.

Cette Bible est dans le domaine public.