Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 141.3
Bible en Swahili de l’est


1 Ee Bwana, nimekuita, unijie hima, Uisikie sauti yangu nikuitapo. 2 Sala yangu ipae mbele zako kama uvumba, Kuinuliwa mikono yangu kama dhabihu ya jioni. 3 Ee Bwana, uweke mlinzi kinywani pangu, Mngojezi mlangoni pa midomo yangu. 4 Usiuelekeze moyo wangu kunako jambo baya, Nisiyazoelee matendo yasiyofaa, Pamoja na watu watendao maovu; Wala nisile vyakula vyao vya anasa. 5 Mwenye haki na anipige, itakuwa fadhili; Anikemee, itakuwa kama mafuta kichwani; Kichwa changu kisikatae, Maana siachi kusali kati ya mabaya yao. 6 Makadhi wao wakiangushwa kando ya genge, Watayasikia maneno yangu, maana ni matamu. 7 Kama kupasua kuni na kuzichanja juu ya nchi, Ndivyo ilivyo mifupa yetu mdomoni pa kuzimu. 8 Macho yangu yanakuelekea Wewe, MUNGU Bwana, Nimekukimbilia Wewe, usiniache nafsi yangu. 9 Unilinde na mtego walionitegea, Na matanzi yao watendao maovu. 10 Wabaya na waanguke katika nyavu zao wenyewe, Pindi mimi ninapopita salama.

Cette Bible est dans le domaine public.