Chapitre 127 Chapitre 129Bénédiction du foyer de l’homme fidèle
1 Heri kila mtu amchaye Bwana, Aendaye katika njia yake.
2 Taabu ya mikono yako hakika utaila; Utakuwa heri, na kwako kwema.
3 Mkeo atakuwa kama mzabibu uzaao, Vyumbani mwa nyumba yako. Wanao kama miche ya mizeituni Wakiizunguka meza yako.
4 Tazama, atabarikiwa hivyo, yule amchaye Bwana. 5 Bwana akubariki toka Sayuni; Uone uheri wa Yerusalemu siku zote za maisha yako;
6 Naam, ukawaone wana wa wanao. Amani ikae na Israeli.
Vous êtes actuellement sur une version optimisée pour mobile, si vous souhaitez basculer sur la version complète suivez le lien suivant : Psaumes 128.4 (Lemaîtstre de Sacy)
Cette Bible est dans le domaine public.