1  Akaniambia, Mwanadamu, simama kwa miguu yako, nami nitasema nawe. 
Daniel 10.11  Ezéchiel 4.1  Ezéchiel 5.1  Actes 9.6  Ezéchiel 3.1  
 2  Naye aliposema nami, roho ikaniingia, ikanisimamisha; nikamsikia yeye aliyesema nami. 
Ezéchiel 3.24  Daniel 8.18  1 Samuel 16.13  Nombres 11.25-11.26  Juges 13.25  
 3  Akaniambia, Mwanadamu, nakutuma kwa wana wa Israeli, kwa mataifa wanaoasi, walioniasi mimi; wao na baba zao wamekosa juu yangu, naam, hata hivi leo. 
Jérémie 3.25  1 Samuel 8.7-8.8  2 Chroniques 36.15-36.16  Jean 20.21-20.22  Romains 10.15  
 4  Na wana hao wana nyuso zisizo na haya, na mioyo yao ni migumu. Mimi nakutuma kwa hao; nawe utawaambia, Bwana MUNGU asema hivi. 
Ezéchiel 3.7  Psaumes 95.8  Esaïe 48.4  Jérémie 6.15  Jérémie 5.3  
 5  Nao, kwamba watasikia, au kwamba hawataki kusikia, (maana ndio nyumba ya kuasi hao), hata hivyo watajua ya kuwa nabii amekuwako miongoni mwao. 
Ezéchiel 33.33  Ezéchiel 3.27  Ezéchiel 2.7  Matthieu 10.12-10.15  Jean 15.22  
 6  Na wewe, mwanadamu, usiwaogope hao, wala usiyaogope maneno yao, ijapokuwa miiba na michongoma i pamoja nawe, nawe unakaa katikati ya nge; usiyaogope maneno yao, wala usifadhaike kwa sababu ya nyuso zao, wajapokuwa ni nyumba yenye kuasi. 
Jérémie 1.17  Jérémie 1.8  Michée 7.4  Esaïe 9.18  Esaïe 51.12  
 7  Nawe utawaambia maneno yangu, kwamba watasikia, au kwamba hawataki kusikia; maana hao wanaasi sana. 
Ezéchiel 3.10  Jérémie 23.28  Ezéchiel 3.17  Jérémie 1.7  Jérémie 1.17  
 8  Bali wewe, mwanadamu, sikia neno hili ninalokuambia; usiwe wewe mwenye kuasi kama nyumba ile yenye kuasi; funua kinywa chako, ule nikupacho. 
Apocalypse 10.9  Jérémie 15.16  Esaïe 50.5  1 Timothée 4.14-4.16  Lévitique 10.3  
 9  Nami nilipotazama, mkono ulinyoshwa kunielekea; na tazama, gombo la chuo lilikuwa ndani yake. 
Ezéchiel 8.3  Ezéchiel 3.1  Daniel 10.10  Apocalypse 10.8-10.11  Apocalypse 5.1-5.5  
 10  Akalikunjua mbele yangu; nalo lilikuwa limeandikwa ndani na nje; ndani yake yalikuwa yameandikwa maombolezo, na vilio, na ole! 
Apocalypse 8.13  Esaïe 3.11  Apocalypse 9.12  Apocalypse 11.14  Jérémie 36.29-36.32