Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Ezéchiel 2.5
Bible en Swahili de l’est


1 Akaniambia, Mwanadamu, simama kwa miguu yako, nami nitasema nawe.Daniel 10.11 Ezéchiel 3.4 Ezéchiel 4.1 Ezéchiel 5.1 Actes 9.6
2 Naye aliposema nami, roho ikaniingia, ikanisimamisha; nikamsikia yeye aliyesema nami.Ezéchiel 3.24 Daniel 8.18 Ezéchiel 36.27 Ezéchiel 3.14 Joël 2.28-2.29
3 Akaniambia, Mwanadamu, nakutuma kwa wana wa Israeli, kwa mataifa wanaoasi, walioniasi mimi; wao na baba zao wamekosa juu yangu, naam, hata hivi leo.Jérémie 3.25 1 Samuel 8.7-8.8 Psaumes 106.16-106.21 Psaumes 106.32-106.40 Actes 7.51
4 Na wana hao wana nyuso zisizo na haya, na mioyo yao ni migumu. Mimi nakutuma kwa hao; nawe utawaambia, Bwana MUNGU asema hivi.Ezéchiel 3.7 Jérémie 6.15 Jérémie 5.3 Psaumes 95.8 Esaïe 48.4
5 Nao, kwamba watasikia, au kwamba hawataki kusikia, (maana ndio nyumba ya kuasi hao), hata hivyo watajua ya kuwa nabii amekuwako miongoni mwao.Ezéchiel 33.33 Ezéchiel 3.27 Actes 13.46 Ezéchiel 2.7 Matthieu 10.12-10.15
6 Na wewe, mwanadamu, usiwaogope hao, wala usiyaogope maneno yao, ijapokuwa miiba na michongoma i pamoja nawe, nawe unakaa katikati ya nge; usiyaogope maneno yao, wala usifadhaike kwa sababu ya nyuso zao, wajapokuwa ni nyumba yenye kuasi.Michée 7.4 Jérémie 1.17 Jérémie 1.8 2 Samuel 23.6-23.7 Esaïe 9.18
7 Nawe utawaambia maneno yangu, kwamba watasikia, au kwamba hawataki kusikia; maana hao wanaasi sana.Ezéchiel 3.10 Jérémie 23.28 Ezéchiel 3.17 Jérémie 1.7 Jérémie 1.17
8 Bali wewe, mwanadamu, sikia neno hili ninalokuambia; usiwe wewe mwenye kuasi kama nyumba ile yenye kuasi; funua kinywa chako, ule nikupacho.Apocalypse 10.9 Jérémie 15.16 Esaïe 50.5 Ezéchiel 3.10 Nombres 20.24
9 Nami nilipotazama, mkono ulinyoshwa kunielekea; na tazama, gombo la chuo lilikuwa ndani yake.Ezéchiel 8.3 Apocalypse 10.8-10.11 Apocalypse 5.1-5.5 Ezéchiel 3.1 Daniel 10.10
10 Akalikunjua mbele yangu; nalo lilikuwa limeandikwa ndani na nje; ndani yake yalikuwa yameandikwa maombolezo, na vilio, na ole!Apocalypse 8.13 Esaïe 3.11 Habakuk 2.2 Apocalypse 9.12 Apocalypse 11.14

Cette Bible est dans le domaine public.