Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Ezéchiel 15.3
Bible en Swahili de l’est


1 Neno la Bwana likanijia, kusema, 2 Mwanadamu, mzabibu una sifa gani kuliko mti mwingine, au tawi la mzabibu lililokuwa kati ya miti ya msituni?Esaïe 5.1-5.7 Osée 10.1 Psaumes 80.8-80.16 Jean 15.1-15.6 Jérémie 2.21
3 Je! Mti wake waweza kutwaliwa, ili kufanya kazi yo yote? Watu waweza kufanya chango kwa huo, ili kutundika chombo cho chote?Marc 9.50 Matthieu 5.13 Luc 14.34-14.35 Jérémie 24.8
4 Tazama, watupwa motoni kwa kuni moto umeziteketeza ncha zake zote mbili, nao umeteketea katikati, je! Wafaa kwa kazi yo yote?Jean 15.6 Esaïe 27.11 Ezéchiel 19.14 Esaïe 1.31 Malachie 4.1
5 Tazama, ulipokuwa mzima, haukufaa kwa kazi yo yote; sembuse ukiisha kuliwa na moto, na kuteketea; je! Waweza kufaa kwa kazi yo yote?Jérémie 3.16
6 Basi Bwana MUNGU asema hivi; Kama mzabibu kati ya miti ya msituni, niliyoupa moto uwe kuni, ndivyo nitakavyowatoa wakaao Yerusalemu.Jérémie 24.8-24.10 Jérémie 7.20 Jérémie 21.7 Ezéchiel 17.3-17.10 Ezéchiel 15.2
7 Nami nitaukaza uso wangu juu yao; nao watatoka motoni, lakini moto utawateketeza; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana, nitakapoukaza uso wangu juu yao.Ezéchiel 14.8 Esaïe 24.18 Amos 9.1-9.4 Psaumes 34.16 1 Rois 19.17
8 Nami nitaifanya nchi kuwa ukiwa, kwa sababu wamekosa, asema Bwana MUNGU.Ezéchiel 6.14 Jérémie 25.10-25.11 Ezéchiel 14.13-14.21 2 Chroniques 36.14-36.16 Sophonie 1.18

Cette Bible est dans le domaine public.