1  Ni nani aliyesadiki habari tuliyoileta? Na mkono wa Bwana amefunuliwa nani? 
Jean 12.38  Romains 10.16-10.17  Ephésiens 1.18-1.19  Romains 1.16-1.18  Esaïe 51.9  
 2  Maana alikua mbele zake kama mche mwororo, Na kama mzizi katika nchi kavu; Yeye hana umbo wala uzuri; Na tumwonapo hana uzuri hata tumtamani. 
Esaïe 52.14  Philippiens 2.6-2.7  Esaïe 11.1  Marc 6.3  Jean 9.28-9.29  
 3  Alidharauliwa na kukataliwa na watu; Mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko; Na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao, Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu. 
Esaïe 49.7  Jean 1.10-1.11  Esaïe 53.10  Marc 14.34  Zacharie 11.12-11.13  
 4  Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa. 
1 Pierre 2.24  Matthieu 8.17  Galates 3.13  1 Jean 2.2  1 Pierre 3.18  
 5  Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona. 
1 Pierre 2.24-2.25  1 Pierre 3.18  Romains 5.6-5.10  Matthieu 20.28  Romains 4.25  
 6  Sisi sote kama kondoo tumepotea; Kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe; Na Bwana ameweka juu yake Maovu yetu sisi sote. 
1 Pierre 2.25  1 Pierre 3.18  Psaumes 119.176  Romains 4.25  Romains 3.10-3.19  
 7  Alionewa, lakini alinyenyekea, Wala hakufunua kinywa chake; Kama mwana-kondoo apelekwaye machinjoni, Na kama vile kondoo anyamazavyo Mbele yao wakatao manyoya yake; Naam, hakufunua kinywa chake. 
Actes 8.32-8.33  Matthieu 26.63  Marc 14.61  1 Pierre 2.23  Jean 19.9  
 8  Kwa kuonewa na kuhukumiwa aliondolewa; Na maisha yake ni nani atakayeisimulia? Maana amekatiliwa mbali na nchi ya walio hai; Alipigwa kwa sababu ya makosa ya watu wangu. 
Actes 8.33  Daniel 9.26  Esaïe 53.12  Jean 19.7  1 Pierre 3.18  
 9  Wakamfanyia kaburi pamoja na wabaya; Na pamoja na matajiri katika kufa kwake; Ingawa hakutenda jeuri, Wala hapakuwa na hila kinywani mwake. 
Matthieu 27.57-27.60  Hébreux 4.15  1 Pierre 2.22  1 Jean 3.5  Jean 19.38-19.42  
 10  Lakini Bwana aliridhika kumchubua; Amemhuzunisha; Utakapofanya nafsi yake kuwa dhabihu kwa dhambi, Ataona uzao wake, ataishi siku nyingi, Na mapenzi ya Bwana yatafanikiwa mkononi mwake; 
Hébreux 13.10-13.12  Matthieu 17.5  Zacharie 13.7  Luc 1.33  Actes 2.24-2.28  
 11  Ataona mazao ya taabu ya nafsi yake, na kuridhika. Kwa maarifa yake mtumishi wangu mwenye haki Atawafanya wengi kuwa wenye haki; Naye atayachukua maovu yao. 
Romains 5.18-5.19  Esaïe 53.4-53.6  Esaïe 53.8  Jean 17.3  Esaïe 45.25  
 12  Kwa hiyo nitamgawia sehemu pamoja na wakuu, Naye atagawanya nyara pamoja nao walio hodari; Kwa sababu alimwaga nafsi yake hata kufa, Akahesabiwa pamoja na hao wakosao. Walakini alichukua dhambi za watu wengi, Na kuwaombea wakosaji. 
Luc 22.37  Marc 15.27  Luc 23.32-23.34  Daniel 2.45  Esaïe 52.13