Récompense et certitude du juste
 1  Mungu, unihifadhi mimi, Kwa maana nakukimbilia Wewe. 
Psaumes 56.1  Psaumes 17.8  Esaïe 26.3-26.4  Psaumes 60.1  Psaumes 84.12  
 2  Nimemwambia Bwana, Ndiwe Bwana wangu; Sina wema ila utokao kwako. 
Zacharie 13.9  Psaumes 31.14  Psaumes 91.2  Psaumes 73.25  Psaumes 27.8  
 3  Watakatifu waliopo duniani ndio Walio bora, Hao ndio niliopendezwa nao. 
Malachie 3.17  Tite 3.8  Hébreux 6.10  Cantique 7.10  Proverbes 13.20  
 4  Huzuni zao zitaongezeka Wambadilio Mungu kwa mwingine; Sitazimimina sadaka zao za damu, Wala kuyataja majina yao midomoni mwangu. 
Exode 23.13  Josué 23.7  Psaumes 32.10  Jonas 2.8  Psaumes 106.37-106.38  
 5  Bwana ndiye fungu la posho langu, Na la kikombe changu; Wewe unaishika kura yangu. 
Psaumes 73.26  Psaumes 23.5  Lamentations 3.24  Psaumes 142.5  Psaumes 119.57  
 6  Kamba zangu zimeniangukia mahali pema, Naam, nimepata urithi mzuri. 
Jérémie 3.19  Psaumes 78.55  Romains 8.17  Jean 20.17  1 Corinthiens 3.21-3.23  
 7  Nitamhimidi Bwana aliyenipa shauri, Naam, mtima wangu umenifundisha usiku. 
Psaumes 77.6  Psaumes 42.8  Psaumes 73.24  Psaumes 17.3  Esaïe 48.17  
 8  Nimemweka Bwana mbele yangu daima, Kwa kuwa yuko kuumeni kwangu, sitaondoshwa. 
Actes 2.25-2.28  Psaumes 110.5  Psaumes 121.5  Psaumes 73.23  Psaumes 73.26  
 9  Kwa hiyo moyo wangu unafurahi, Nao utukufu wangu unashangilia, Naam, mwili wangu nao utakaa kwa kutumaini. 
Psaumes 30.12  Psaumes 57.8  Proverbes 14.32  Psaumes 108.1  Jacques 3.5-3.9  
 10  Maana hutakuachia kuzimu nafsi yangu, Wala hutamtoa mtakatifu wako aone uharibifu. 
Psaumes 49.15  Actes 13.35-13.38  Apocalypse 1.18  Apocalypse 20.13  Actes 2.27-2.31  
 11  Utanijulisha njia ya uzima; Mbele za uso wako ziko furaha tele; Na katika mkono wako wa kuume Mna mema ya milele. 
Actes 2.28  Apocalypse 7.15-7.17  Psaumes 21.4-21.6  Psaumes 36.7-36.8  Psaumes 17.15