1 Mungu, unihifadhi mimi, Kwa maana nakukimbilia Wewe.
Psaumes 56.1  Psaumes 17.8  Jérémie 17.7-17.8  Psaumes 7.1  Psaumes 9.10  
 2 Nimemwambia Bwana, Ndiwe Bwana wangu; Sina wema ila utokao kwako.
Zacharie 13.9  Psaumes 31.14  Psaumes 91.2  Psaumes 73.25  Job 22.2-22.3  
 3 Watakatifu waliopo duniani ndio Walio bora, Hao ndio niliopendezwa nao.
Tite 3.8  Hébreux 6.10  Malachie 3.17  Actes 9.13  Proverbes 8.31  
 4 Huzuni zao zitaongezeka Wambadilio Mungu kwa mwingine; Sitazimimina sadaka zao za damu, Wala kuyataja majina yao midomoni mwangu.
Exode 23.13  Psaumes 32.10  Josué 23.7  Jonas 2.8  Esaïe 66.3  
 5 Bwana ndiye fungu la posho langu, Na la kikombe changu; Wewe unaishika kura yangu.
Psaumes 73.26  Psaumes 23.5  Lamentations 3.24  Psaumes 119.57  Psaumes 142.5  
 6 Kamba zangu zimeniangukia mahali pema, Naam, nimepata urithi mzuri.
Jérémie 3.19  Psaumes 78.55  Hébreux 12.2  2 Timothée 2.12  Psaumes 21.1-21.3  
 7 Nitamhimidi Bwana aliyenipa shauri, Naam, mtima wangu umenifundisha usiku.
Psaumes 42.8  Psaumes 73.24  Psaumes 77.6  Psaumes 17.3  Esaïe 48.17  
 8 Nimemweka Bwana mbele yangu daima, Kwa kuwa yuko kuumeni kwangu, sitaondoshwa.
Actes 2.25-2.28  Psaumes 110.5  Psaumes 121.5  Psaumes 73.23  Psaumes 73.26  
 9 Kwa hiyo moyo wangu unafurahi, Nao utukufu wangu unashangilia, Naam, mwili wangu nao utakaa kwa kutumaini.
Psaumes 30.12  Psaumes 57.8  Psaumes 4.7-4.8  Actes 2.26  Job 14.14-14.15  
 10 Maana hutakuachia kuzimu nafsi yangu, Wala hutamtoa mtakatifu wako aone uharibifu.
Psaumes 49.15  Actes 13.35-13.38  Apocalypse 20.13  Actes 2.27-2.31  Apocalypse 1.18  
 11 Utanijulisha njia ya uzima; Mbele za uso wako ziko furaha tele; Na katika mkono wako wa kuume Mna mema ya milele.Actes 2.28  Apocalypse 7.15-7.17  Psaumes 21.4-21.6  Psaumes 36.7-36.8  2 Corinthiens 4.17