Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 121.3
Bible en Swahili de l’est


1 Nitayainua macho yangu niitazame milima, Msaada wangu utatoka wapi? 2 Msaada wangu u katika Bwana, Aliyezifanya mbingu na nchi. 3 Asiuache mguu wako usogezwe; Asisinzie akulindaye; 4 Naam, hatasinzia wala hatalala usingizi, Yeye aliye mlinzi wa Israeli. 5 Bwana ndiye mlinzi wako; Bwana ni uvuli mkono wako wa kuume. 6 Jua halitakupiga mchana, Wala mwezi wakati wa usiku. 7 Bwana atakulinda na mabaya yote, Atakulinda nafsi yako. 8 Bwana atakulinda utokapo na uingiapo, Tangu sasa na hata milele.

Cette Bible est dans le domaine public.