Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 130.7
Bible en Swahili de l’est


1 Ee Bwana, toka vilindini nimekulilia. 2 Bwana, uisikie sauti yangu. Masikio yako na yaisikilize Sauti ya dua zangu. 3 Bwana, kama Wewe ungehesabu maovu, Ee Bwana, nani angesimama? 4 Lakini kwako kuna msamaha, Ili Wewe uogopwe. 5 Nimemngoja Bwana, roho yangu imengoja, Na neno lake nimelitumainia. 6 Nafsi yangu inamngoja Bwana, Kuliko walinzi waingojavyo asubuhi, Naam, walinzi waingojao asubuhi. 7 Ee Israeli, umtarajie Bwana; Maana kwa Bwana kuna fadhili, Na kwake kuna ukombozi mwingi. 8 Yeye atamkomboa Israeli na maovu yake yote.

Cette Bible est dans le domaine public.