Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 12.8
Bible en Swahili de l’est


1 Bwana, uokoe, maana mcha Mungu amekoma, Maana waaminifu wametoweka katika wanadamu. 2 Husemezana yasiyofaa kila mtu na mwenziwe, Wenye midomo ya kujipendekeza; Husemezana kwa mioyo ya unafiki; 3 Bwana ataikata midomo yote ya kujipendekeza, Nao ulimi unenao maneno ya kiburi; 4 Waliosema, Kwa ndimi zetu tutashinda; Midomo yetu ni yetu wenyewe, Ni nani aliye bwana juu yetu? 5 Kwa ajili ya kuonewa kwao wanyonge, Kwa ajili ya kuugua kwao wahitaji, Sasa nitasimama, asema Bwana, Nitamweka salama yeye wanayemfyonya. 6 Maneno ya Bwana ni maneno safi, Ni fedha iliyojaribiwa kalibuni juu ya nchi; Iliyosafishwa mara saba. 7 Wewe, Bwana, ndiwe utakayetuhifadhi, Utatulinda na kizazi hiki milele. 8 Wasio haki hutembea pande zote, Ufisadi ukitukuka kati ya wanadamu.

Cette Bible est dans le domaine public.