Accueil  /  Bible  /  Bible en Swahili de l’est  /  Jérémie 45

La Bible Bible en Swahili de l’est

Jérémie 45

Un clic sur un verset envoie vers le comparateur de versions.

Chapitre 44 Chapitre 46

Sort de Baruc

1 Neno hili ndilo ambalo Yeremia, nabii, alimwambia Baruku, mwana wa Neria, alipoyaandika maneno haya katika kitabu kwa kinywa cha Yeremia, mwaka wa nne wa Yehoyakimu, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda, kusema, 2 Bwana, Mungu wa Israeli, akuambia wewe Ee Baruku; 3 Ulisema, Ole wangu! Kwa maana Bwana ameongeza huzuni pamoja na maumivu yangu. Nimechoka kwa ajili ya kuugua kwangu, wala sioni raha. 4 Basi, mwambie hivi, Bwana asema hivi, Tazama, niliyoyajenga nitayabomoa, na niliyoyapanda nitayang’oa; na haya yatakuwa katika nchi yote. 5 Je! Unajitafutia mambo makuu? Usiyatafute; kwa maana tazama, nitaleta mabaya juu ya wote wenye mwili, asema Bwana; lakini roho yako nitakupa iwe nyara, katika mahali pote utakapokwenda.


Vous êtes actuellement sur une version optimisée pour mobile, si vous souhaitez basculer sur la version complète suivez le lien suivant : Jérémie 45.1 (Lemaîtstre de Sacy)

Cette Bible est dans le domaine public.