Un clic sur un verset envoie vers le comparateur de versions.
Genèse 36.20 Bible en Swahili de l’est
1 Hivi ndivyo vizazi vya Esau, ndiye Edomu. 2 Esau alitwaa binti za Kanaani, kuwa wakeze; Ada, binti Eloni, Mhiti, na Oholibama, binti Ana, binti Sibeoni, Mhivi; 3 na Basemathi, binti Ishmaeli, nduguye Nebayothi. 4 Ada akamzalia Esau Elifazi; na Basemathi alizaa Reueli. 5 Oholibama alizaa Yeushi, na Yalamu, na Kora. Hao ndio wana wa Esau aliozaliwa katika nchi ya Kanaani. 6 Esau akawatwaa wakeze, na wanawe, na binti zake, na watu wote wa nyumbani mwake, na ng’ombe zake, na wanyama wake wote, na mali yake yote, aliyoyapata katika nchi ya Kanaani; akaenda mpaka nchi iliyo mbali na Yakobo nduguye. 7 Maana mali yao yalikuwa mengi wasiweze kukaa pamoja, wala haikuweza nchi ya kusafiri kwao kuwachukua, kwa sababu ya wanyama wao. 8 Esau akakaa katika mlima Seiri, Esau ndiye Edomu. 9 Hivi ni vizazi vya Esau, baba ya Edomu katika mlima Seiri. 10 Haya ndiyo majina ya wana wa Esau; Elifazi, mwana wa Ada mkewe Esau. Reuli, mwana wa Basemathi, mkewe Esau. 11 Na wana wa Elifazi, ni Temani na Omari, na Sefo, na Gatamu, na Kenazi. 12 Na Timna alikuwa suria wa Elifazi, mwana wa Esau; naye akamzalia Elifazi Amaleki. Hao ndio wana wa Ada, mkewe Esau. 13 Na hawa ni wana wa Reueli, Nahathi, na Zera, na Shama na Miza. Hao walikuwa wana wa Basemathi, mkewe Esau. 14 Na hawa ni wana wa Oholibama, binti Ana, binti Sibeoni, mkewe Esau; akamzalia Esau, Yeushi, na Yalamu, na Kora. 15 Hawa ndio majumbe wao wana wa Esau; wana wa Elifazi, mzaliwa wa kwanza wa Esau; jumbe Temani, jumbe Omari, jumbe Sefo, jumbe Kenazi, 16 jumbe Kora, jumbe Gatamu, jumbe Amaleki. Hao ndio majumbe, waliotoka kwa Elifazi katika nchi ya Edomu. Hao ni wana wa Ada. 17 Na hawa ni wana wa Reueli, mwanawe Esau; jumbe Nahathi, jumbe Zera, jumbe Shama, jumbe Miza. Hao ndio majumbe waliotoka kwa Reueli katika nchi ya Edomu. Hao ni wana wa Basemathi, mkewe Esau. 18 Na hawa ni wana wa Oholibama, mkewe Esau; jumbe Yeushi, jumbe Yalamu, jumbe Kora. Hao ndio majumbe waliotoka kwa Oholibama, binti Ana, mkewe Esau. 19 Hao ni wana wa Esau, na hao ndio majumbe wao; naye Esau ndiye Edomu.20 Hawa ni wana wa Seiri, Mhori, wenyeji wa nchi ile; Lotani, na Shobali, na Sibeoni, na Ana,21 na Dishoni, na Eseri, na Dishani. Hao ndio majumbe waliotoka katika Wahori, wana wa Seiri, katika nchi ya Edomu. 22 Na wana wa Lotani, ni Hori, na Hemamu; na umbu lake Lotani ni Timna. 23 Na hawa ni wana wa Shobali, Alvani, na Manahathi, na Ebali, na Shefo, na Onamu. 24 Na hawa ni wana wa Sibeoni, Aya, na Ana; ni yule Ana aliyeona chemchemi za maji ya moto katika jangwa, alipokuwa akichunga punda za Sibeoni babaye. 25 Na hawa ni wana wa Ana, Dishoni, na Oholibama, binti Ana. 26 Na hawa ni wana wa Dishoni, Hemdani, na Eshbani, na Ithrani, na Kerani. 27 Na hawa ni wana wa Eseri, Bilhani, na Zaawani, na Akani. 28 Na hawa ni wana wa Dishani, Usi, na Arani. 29 Hawa ndio majumbe waliotoka katika Wahori; jumbe Lotani, jumbe Shobali, jumbe Sibeoni, jumbe Ana, 30 jumbe Dishoni, jumbe Eseri jumbe Dishani. Hao ndio majumbe waliotoka katika Wahori, kwa habari za majumbe yao, katika nchi ya Seiri. 31 Na hawa ndio wafalme waliomiliki katika nchi ya Edomu, kabla ya kumiliki mfalme ye yote juu ya wana wa Israeli. 32 Bela wa Beori alimiliki katika Edomu, na jina la mji wake ni Dinhaba. 33 Akafa Bela, akamiliki Yobabu mwana wa Zera, wa Bosra, badala yake. 34 Akafa Yobabu, akamiliki Hushamu, wa nchi ya Watemani, badala yake. 35 Akafa Hushamu, akamiliki Hadadi wa Bedadi badala yake, naye ndiye aliyepiga Midiani katika nyika ya Moabu, na jina la mji wake ni Avithi. 36 Akafa Hadadi, akamiliki Samla wa Masreka badala yake. 37 Akafa Samla, na Shauli wa Rehobothi, ulio karibu na mto, akamiliki badala yake. 38 Akafa Shauli, akamiliki Baal-hanani, mwana wa Akbori, badala yake. 39 Akafa Baal-hanani, mwana wa Akbori, akamiliki Hadadi badala yake; na jina la mji wake ni Pau; na jina la mkewe ni Mehetabeli, binti Matredi, binti Mezahabu. 40 Na hayo ndiyo majina ya majumbe waliotoka kwa Esau, kufuata jamaa zao, na mahali pao, kwa majina yao. Jumbe Timna, jumbe Alva, jumbe Yethethi, 41 jumbe Oholibama, jumbe Ela, jumbe Pinoni, 42 jumbe Kenazi, jumbe Temani, jumbe Mibsari, 43 jumbe Magdieli, jumbe Iramu. Hao ndio majumbe wa Edomu, kufuata makao yao, katika nchi ya mamlaka yao. Naye huyo ndiye Esau, baba ya Edomu.