Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Proverbes 30.29
Bible en Swahili de l’est


1 Maneno ya Aguri bin Yake; mausia mtu huyu aliyomwambia Ithieli, naam, Ithieli na Ukali.Proverbes 31.1 2 Pierre 1.19-1.21
2 Hakika nimekuwa kama mnyama, wala si mtu; Wala sina ufahamu wa mwanadamu;Psaumes 73.22 Jérémie 10.14 Proverbes 5.12 Psaumes 92.6 Esaïe 6.5
3 Wala sikujifunza hekima; Wala sina maarifa ya kumjua Mtakatifu.Proverbes 9.10 Esaïe 6.10 Job 11.7-11.9 Esaïe 57.15 Apocalypse 3.7
4 Ni nani aliyepanda mbinguni na kushuka chini? Ni nani aliyekamata upepo kwa makonzi yake? Ni nani aliyeyafunga maji ndani ya nguo yake? Ni nani aliyefanya imara ncha zote za nchi? Jina lake ni nani? Na ni nani jina la mwanawe, kama wajua?Jean 3.13 Esaïe 53.8 Esaïe 9.6 Exode 34.5-34.7 Esaïe 7.14
5 Kila neno la Mungu limehakikishwa; Yeye ni ngao yao wamwaminio.Psaumes 18.30 Psaumes 12.6 Psaumes 84.11 Psaumes 3.3 Jacques 3.17
6 Usiongeze neno katika maneno yake; Asije akakulaumu, ukaonekana u mwongo.Deutéronome 12.32 Deutéronome 4.2 Apocalypse 22.18-22.19 Job 13.7-13.9 1 Corinthiens 15.15
7 Mambo haya mawili nimekuomba; Usininyime [matatu] kabla sijafa.2 Rois 2.9 Psaumes 27.4 Luc 10.42 1 Rois 3.5-3.9 Psaumes 21.2
8 Uniondolee ubatili na uongo; Usinipe umaskini wala utajiri; Unilishe chakula kilicho kadiri yangu.Matthieu 6.11 Luc 11.3 Psaumes 119.29 1 Timothée 6.6-6.8 Psaumes 62.9-62.10
9 Nisije nikashiba nikakukana, Nikasema, Bwana ni nani? Wala nisiwe maskini sana nikaiba, Na kulitaja bure jina la Mungu wangu.Deutéronome 31.20 Osée 13.6 Job 31.24-31.28 Deutéronome 8.10-8.14 Ezéchiel 16.49-16.50
10 Usimchongee mtumwa kwa bwana wake; Asije akakulaani, ukaonekana una hatia.Daniel 3.8-3.18 1 Samuel 24.9 Romains 14.4 2 Samuel 16.1-16.4 Deutéronome 23.15
11 Kuna kizazi cha watu wamlaanio baba yao; Wala hawambariki mama yao.Proverbes 20.20 Proverbes 30.17 Proverbes 30.12-30.14 Deutéronome 27.16 Exode 21.17
12 Kuna kizazi cha watu walio safi machoni pao wenyewe; Ambao hawakuoshwa uchafu wao.Luc 18.11 Jérémie 2.35 Proverbes 16.2 Esaïe 65.5 Luc 11.39-11.40
13 Kuna kizazi cha watu ambao macho yao yameinuka kama nini! Na kope zao zimeinuka sana.Proverbes 6.17 Esaïe 2.11 Ezéchiel 28.2-28.5 Esaïe 3.16 Daniel 11.36-11.37
14 Kuna kizazi cha watu ambao meno yao ni panga; Na vigego vyao ni kama visu. Ili kuwala maskini waondolewe katika nchi, Na wahitaji katika wanadamu.Psaumes 57.4 Psaumes 3.7 Psaumes 14.4 Job 29.17 Amos 8.4
15 Mruba anao binti wawili, Waliao, Nipe! Nipe! Kuna vitu vitatu visivyoshiba kamwe, Naam, vinne visivyosema, Basi!Proverbes 30.21 Proverbes 30.29 Proverbes 6.16 Esaïe 57.3 Romains 16.18
16 Kuzimu; na tumbo lisilozaa; Nchi isiyoshiba maji; na moto usiosema, Basi!Proverbes 27.20 Habakuk 2.5 Genèse 30.1
17 Jicho la mtu amdhihakiye babaye, Na kudharau kumtii mamaye; Kunguru wa bondeni wataling’oa, Na vifaranga vya tai watalila.Proverbes 23.22 Proverbes 30.11 Deutéronome 21.18-21.21 2 Samuel 21.10 2 Samuel 18.14-18.17
18 Kuna mambo matatu yaliyo ya ajabu kwangu, Naam, kuna manne nisiyoyafahamu.Job 42.3 Psaumes 139.6
19 Mwendo wa tai katika hewa; Na mwendo wa nyoka juu ya mwamba; Mwendo wa merikebu katikati ya bahari; Na mwendo wa mtu pamoja na msichana.Job 39.27 Esaïe 40.31 Exode 22.16
20 Hivyo ndivyo mwendo wa mwanamke mzinifu; Hula, akapangusa kinywa chake, Akasema, Sikufanya uovu.Proverbes 7.13-7.23 Nombres 5.11-5.30 Proverbes 5.6
21 Kwa ajili ya mambo matatu nchi hutetemeka, Naam, kwa ajili ya manne haiwezi kuvumilia. 22 Mtumwa apatapo kuwa mfalme; Mpumbavu ashibapo chakula;Proverbes 19.10 Ecclésiaste 10.7 Proverbes 28.3 1 Samuel 25.10-25.11 Esaïe 3.4-3.5
23 Mwanamke mwenye kuchukiza aolewapo; Na mjakazi aliye mrithi wa bibi yake.Proverbes 27.15 Proverbes 29.21 Proverbes 21.19 Proverbes 21.9 Proverbes 19.13
24 Kuna viumbe vinne duniani vilivyo vidogo; Lakini vina akili nyingi sana.Job 12.7
25 Chungu ni watu wasio na nguvu; Lakini hujiwekea chakula wakati wa hari.Proverbes 6.6-6.8
26 Wibari ni watu dhaifu; Lakini hujifanyia nyumba katika miamba.Psaumes 104.18 Lévitique 11.5
27 Nzige hawana mfalme; Lakini huenda wote pamoja vikosi vikosi.Psaumes 105.34 Joël 1.6-1.7 Exode 10.4-10.6 Joël 2.25 Joël 1.4
28 Mjusi hushika kwa mikono yake; Lakini yumo majumbani mwa wafalme. 29 Kuna watatu wenye mwendo wa kupendeza, Naam, wanne walio na mwendo mzuri. 30 Simba aliye hodari kupita wanyama wote; Wala hajiepushi na aliye yote;Juges 14.18 Nombres 23.24
31 Jimbi aendaye tambo; na beberu; Na mfalme ambaye haasiki.Proverbes 16.14 Proverbes 20.2 Daniel 3.15-3.18
32 Ikiwa umefanya kipumbavu kwa kujikuza; Au ikiwa umewaza mabaya; Basi weka mkono wako juu ya kinywa chako.Job 21.5 Job 40.4 Ecclésiaste 8.3-8.4 Proverbes 26.12 Romains 3.19
33 Kwa maana kupiga maziwa huleta siagi; Na kupiga pua hutokeza damu; kadhalika kuchochea hasira hutokeza ugomvi.Proverbes 29.22 Proverbes 17.14 Proverbes 26.21 Proverbes 15.18 Proverbes 16.28

Cette Bible est dans le domaine public.