Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Job 26.1
Bible en Swahili de l’est


1 Ndipo Ayubu akajibu, na kusema, 2 Jinsi ulivyomsaidia huyo asiye na uwezo! Jinsi ulivyouokoa mkono usio na nguvu!1 Rois 18.27 Job 4.3-4.4 Esaïe 35.3-35.4 Esaïe 41.5-41.7 Psaumes 71.9
3 Jinsi ulivyomshauri huyo asiye na hekima! Na kutangaza ujuzi wa kweli kwa wingi!Job 33.33 Job 13.5 Job 15.8-15.10 Psaumes 71.15-71.18 Psaumes 49.1-49.4
4 Je! Umetamka maneno kwa nani? Kisha ni roho ya nani iliyotoka kwako?1 Rois 22.23-22.24 Ecclésiaste 12.7 Job 20.3 Apocalypse 16.13-16.14 1 Corinthiens 12.3
5 Hao waliokufa watetema Chini ya maji na hao wayakaao.Genèse 6.4 Psaumes 88.10 Ezéchiel 29.3-29.5 Psaumes 104.25-104.26 Job 41.1-41.34
6 Kaburi li wazi mbele yake, Uharibifu nao hauna kifuniko.Proverbes 15.11 Psaumes 139.8 Job 28.22 Hébreux 4.13 Amos 9.2
7 Yeye hutandaza kaskazi juu ya nafasi isiyo na kitu, Na kuutundika ulimwengu pasipo kitu.Job 9.8 Psaumes 104.2-104.5 Genèse 1.1-1.2 Esaïe 40.22 Esaïe 42.5
8 Huyafunga maji ndani ya mawingu yake mazito; Na hilo wingu halipasuki chini yake.Proverbes 30.4 Jérémie 10.13 Esaïe 5.6 Job 38.9 Job 37.11-37.16
9 Husitiri uso wa kiti chake cha enzi, Na kulitandaza wingu lake juu yake.Psaumes 97.2 Habakuk 3.3-3.5 Exode 33.20-33.23 1 Rois 8.12 Exode 34.3
10 Amepiga duara kuwa ni mpaka juu ya uso wa maji, Hata hapo mwanga na giza vinapopakana.Proverbes 8.29 Job 38.8-38.11 Jérémie 5.22 Psaumes 33.7 Esaïe 54.9-54.10
11 Nguzo za mbingu zatetemeka, Na kustaajabu kwa kukemea kwake.1 Samuel 2.8 Job 15.15 Psaumes 18.7 2 Pierre 3.10 Hébreux 12.26-12.27
12 Huichafua bahari kwa uwezo wake, Na kumtema Rahabu kwa akili zake.Esaïe 51.15 Jérémie 31.35 Job 9.13 Psaumes 89.9-89.10 Esaïe 51.9
13 Hizo mbingu hupambwa kwa roho yake; Mkono wake umemchoma nyoka aendaye mbio.Esaïe 27.1 Psaumes 74.13-74.14 Psaumes 104.30 Genèse 1.2 Psaumes 33.6-33.7
14 Tazama, hivi ni viunga tu vya njia zake; Na jinsi yalivyo madogo manong’ono tusikiayo katika habari zake! Lakini ngurumo za uweza wake ni nani awezaye kuelewa nazo?1 Corinthiens 13.9-13.12 Psaumes 139.6 Job 40.9 Esaïe 40.26-40.29 Romains 11.33

Cette Bible est dans le domaine public.